Rais wa
Ufaransa, François Hollande, katika tangazo la Alhamisi Februari 12,
ametangaza kuizia Misri ndege 24 za kivita aina ya Rafale, ikiwa ni
pamoja na vifaa vinavyohusiana na ndege hizo.
Ufaransa na Misri zinatazamiwa kutiliana saini kwenye mkataba
wa mauzo ya ndege hizo Jumatatu Februari 16 katika mji mkuu wa Misri,
Cairo.
Vyombo vya habari vya Ufaransa vimekua vikizungumzia suala hilo la mauzo ya ndege kwa siku kadhaa. Rais François Hollande, amethibitisha katika tangazo alilotoa Alhamisi wiki hii : makubaliano yalifikiwa na Misri kwa mauzo ya ndege 24 za kivita aina ya Rafale, vifaa vinavyohusiana na ndege hizo pamoja na makombora.
Mapema Alhamisi wiki hii, rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sissi alikubali makubaliano hayo na kuruhusu kusafirishwa kwa ndege hizo hadi Misri, hivyo kuhitimisha mkataba wa kiasi chaYuro bilioni 5.2 ambapo Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian atajielekeza Misri kutiliana saini kwa niaba ya Ufaransa na rais wa Misri kwenye mkataba wa mauzo hayo, amesema rais Hollande katika tangazo lililotoleawa Alhamisi wiki hii. Mkataba huo utatiliwa saini Jumatatu Februari 16.
Wiki hii, Sheikh Mohamed ben Zayed al-Nahyan, alipokelewa katika Ikulu ya Elysée, ambapo suala la mauzo ya ndege hizo lilizungumziwa. Falme za Kiarabu zimejikubalisha kutoa pesa hizo za mauzo ya ndege za kivita kwa nchi ya Misri.
Serikali ya Misri inahitaji ndege hizo haraka iwezekanavyo. Hata hivyo Ufaransa imekubali kusafirisha ndege kadhaa kwa minajili ya uzinduzi wa upanuzi wa eneo la Suez uliyopangwa kufanyika katika majira ya joto mwaka 2015.

No comments:
Post a Comment