Shirikisho la Riadha duniani (IAAF)
na Chama Cha kimataifa cha mbio ndefu na fupi za marathon ( AIMS) wamepima na
kupitisha njia zitakazotumika kwa ajili ya mbio za kimataifa za Kilimanjaro
Marathon zitakazofanyika March 1 mkoani Kilimanjaro (Moshi) Kaskazini mwa
Tanzania.
Mbio hizo zinashirikisha wakimbiaji
mahiri kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Kenya, moja ya nchi maarufu katika mchezo
wa riadha Afrika na Dunia kwa ujumla.
Kazi ya upimaji imefanywa na Katibu
wa AIMS, Hugh Jones akisaidiwa na kiongozi wa riadha kutoka Kenya ( Nairobi
Marathon) Michael Hughes na Ibrahim Hussein wa IAAF pamoja na mkurugenzi wa
mbio hizo, John Bayo wa Kilimanjaro Marathon Club.
Kukiwa hakuna mabadiliko makubwa ya
routes zilizotumika mwaka jana, washiriki watapita Mweka Road huku wakipata
fursa ya kuuona Mlima Kilimanjaro, ambao ndio mrefu kuliko yote Barani Afrika,
ikiwa kama sehemu ya kukuza utalii wa ndani pia.
Wafukuza upepo wakichuana
Mbio zitaanza Chuo Cha Ushirika
mapema saa 6.30 asubuhi, huku kukiwa na mbio za full Marathon, half marathon
kwa wakimbiaji wa kawaida, half Marathon tena kwa watu wenye ulemavu na
Kilometa 5 kwa ajili ya afya.
No comments:
Post a Comment