Monday, 16 February 2015
TAARIFA ZA CHANZO CHA KIFO CHA DINGI AKE' DULLY NA MAZIKO ...>
Marehemu Mzee Abby Sykes ambaye ni Baba mzazi wa mwimbaji wa Bongo Fleva Prince Dullysykes, alifariki saa 8 mchana February 15 2015 akiwa hospitali ya taifa Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Dullysykes ameongea na millardayo.com ikiwa ni pamoja na kuelezea kitu kilichosababisha umauti wa baba yake ambapo ameanza kwa kusema
"Mzee alikua ana vidonda katika miguu na ndiyo chanzo kikubwa, sumu ikasambaa ikasababisha kifo chake, vidonda vilishindwa kupona kwa ajili ya moshi wa sigara ila zaidi hakuwa na tatizo jingine lolote manake baba yangu alikua strong"
‘Alianza kuugua vidonda miezi minne iliyopita, miezi miwili alikua anavumilia tu lakini miezi miwili ya mwishoni ndiyo vilizidi kumsumbua, mazishi tunategemea kuyafanya February 16 2015 saa kumi jioni kwenye makaburi ya Kisutu lakini safari ya kwenda msikitini tutaanza saa 7 mchana‘ – Dully.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment