MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema) ameng’ara katika mbio
za urais mwaka 2015 akipata asilimia 18 tofauti na wagombea wengine
wanaotajwa kugombea nafasi hiyo kupitia muungano wa vyama vinne
vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), utafiti umebaini.
Takwimu hizo zilitolewa na Asasi ya Utafiti wa Elimu Tanzania ( TEDRO)
kwa lengo la kutathmini ushiriki wa vijana katika siasa kama wagombea na
namna ambavyo vijana wanavyopokewa katika jamii.
Akitoa ripoti hiyo Dar es Salaam jana Mkurugenzi wa TEDRO, Jacob Kateri,
alisema takwimu hizo zinaonesha kuwa Zitto ni kijana anayepewa nafasi
kubwa endapo atapeperusha bendera ya Ukawa.
Katika utafiti huo Zitto anafuatiwa na Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia
kwa asilimia 16, Tundu Lissu (14), John Mnyika (7), David Kafulila (6),
Julius Mtatiro (4), Moses Machali (4) na Joshua Nasari (2).
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu (bara) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Mwigulu Nchemba alionekana kuwapiku wenzake kupitia chama hicho kwa
asilimia 38, akifuatiwa na Dk. Emmanuel Nchimbi (26), Januari Makamba
(24), William Ngeleja (11), Lazaro Nyalandu (100, Hamis Kigwangala (7),
Deo Filikunjombe (5) na Esther Bulaya (2).
Kateri alisema utafiti huo ulilenga kuchambua malengo mahususi manne
ambayo ni ushiriki wa vijana katika siasa kama wagombea, mchango wa
wanasiasa vijana katika kufuata misingi ya utawala bora, uwajibikaji na
utelezaji wa ahadi za wagombea.
Kateri alisema utafiti huo uliweka sababu mbalimbali ambazo ni kichocheo
kwa vijana kuingia katika siasa zikiwemo uzalendo asilimia 67 kimbilio
baada ya kukosa ajira (57), uwezo mdogo wa watangulizi wao katika nafasi
husika (60), mafanikio ya wanasiasa vijana walio mahiri (72), vyama vya
siasa kuwapa nafasi vijana katika vyama vyao (59) na kukubalika kwa
vijana sababu ni vijana 63.
“Utafiti huu umeandaliwa na kufanyika Tanzania Bara na ulifanyika katika
wilaya 18 na utafikia kila kanda ukiwa umehusisha wilaya moja hadi tatu
huku kila wilaya vimehojiwa vijiji vitatu na watu 15.
No comments:
Post a Comment