Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alitoa agizo hilo
alipozindua mpango wa Serikali wa kukuza stadi za Kusoma, Kuandika na
Kuhesabu (KKK) katika Chuo kikuu cha Dodoma juzi.
Alisema Serikali itakuwa haitendi haki kwa
wananfunzi wake ambao wamesoma kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo na
mwisho wake wakazuiwa kufanya mitihani ya kumaliza chuo kwa sababu za
kukosa ada.
Pinda alimwagiza Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(Tamisemi), Sifuni Mchome kuviandikia barua vyuo hivyo ili wanafunzi
wasizuiwe kufanya mitihani.
“Kuna baadhi ya wanafunzi kutokana na matatizo ya
kwenye familia zao hukosa fedha za kufanyia mtihani, kwa hiyo tuwazuie
eti kwa sababu tu hawajalipa ada? Hapana, tutakuwa hatuwatendei haki
vijana wetu ambao wamejitahidi kusoma kwa miaka mitatu na mwisho wake
wakose kufanya mitihani.
Kuhusiana na mpango wa KKK, Pinda alisema ni ni
mzuri kama utasimamiwa vizuri kwani unaweza kuleta matokeo mazuri katika
mfumo wa elimu nchini. Alisema mpango huo unatakiwa kusimamiwa na
Serikali Kuu ambao ni watunga sera na Serikali za Mitaa ambako ndipo
kuna shule za chekechea, msingi na sekondari.
Naibu Waziri wa Tamisemi (Elimu), Kassim Majaliwa
alisema mpango wa KKK ni lazima utawafikia wakuu wa mikoa, watendaji wa
halmashauri na madiwani ili iwe ni ajenda yao ya mara kwa mara.
Mpango wa KKK ni wa mwaka 2014/16 na unatekelezwa katika shule zote za misingi kwa watoto walioko darasa la kwanza na la pili.
No comments:
Post a Comment