Sunday, 1 February 2015

UCHAGUZI MKUU 2015 NA UMUHIMU WA LOWASSA ..!



Kwa  sasa  nazungumza  kama  mtanzania  mzalendo, sababu  itikadi  ya  uzalendo  ni  moja  tu  nayo  ni  mapenzi  kwa  kile  unachokiamini  kuwa  ni  cha  kweli.........

Uzalendo  wa  nchi  haupaswi   kutawaliwa  na  itikadi  wala  ushabiki  wa  kundi  moja  dhidi  ya kundi  jingine  la  wananchi.

Kilichomuhimu  katika  uzalendo  wa  kweli  kwa  nchi  ni  upendo  wa  kilichobora  katika  kuijenga  na  kuiimarisha  nchi...

Mwaka  huu  nchi  yetu  inafanya  uchaguzi  mkuu  kwa  ajili  ya  kupata  viongozi  wapya  wa  awamu  ya  tano tangu  ianze  kujitawala.

Pamoja  na  uchaguzi  huo  kuhusisha  wabunge  na  madiwani, anayelengwa  zaidi  ni  kiongozi  mkuu  wa  nchi, Rais.Huyo  ndiye  niliyedhamilia  kumjadili  hapa.

Kwa  vile  watanzania  kiitikadi  tumegawanyika  katika  vyama  vingi  vya  siasa,ni  lazima  anayefaa  kuwa  kiongozi  wetu  mkuu  atoke  kwenye  chama  kimojawapo, au  pengine  hata  bila  chama  kulingana  na  mfumo  utakaokubalika  kuendesha  uchaguzi  huo  ifikapo  mwishoni  mwa  mwaka  huu.

Lakini  kwa  vile  watanzania  tuko  wengi, zaidi  ya  watu  milioni 45,kitu  ambacho  ni  wazi kinaleta  ugumu  wa  kutambuana  harakaharaka  na  kumjua  ni  yupi  anayefaa  kuwa  kiongozi  wetu  mkuu  kati  yetu, inatuwia  rahisi  kumwangalia  mtu  huyo  kati  ya  wale  walioonyesha  nia  ya  kuitaka  nafasi  hiyo.

Mpaka  sasa  walioonyesha  nia  au  kutangaza  nia  ya  wazi  ya  kuutaka  ukuu  wa  nchi  yetu  ni  makada  wa  chama  tawala,CCM.

Kwa  maana  hiyo  nisieleweke  vibaya  kwa  kuwaangalia  hao  walioonyesha  nia.Ntakuwa  sitendi  haki  kuwasemea  ambao  hawajawa  tayari  kuonysha  nia  za  kutaka  kuubeba  mzigo  huo, urais  ni  mzigo  mzito.

Kati  ya  makada  hao  wa  CCM  walioonyesha  nia,tukiziweka  itikadi  zetu  pembeni, tunaweza  kumpata  aliyebora  zaidi  ya  wengine  wote, vigezo  vya  kumpata  viko  wazi  kama  ntakavyoonyesha  hapo  chini.

Kwanza  jambo  lililorahisisha  kazi  ya  kumweka  wazi  na  kumtambua  aliye  bora  zaidi  ya  wengine  ni  mbinu  zinazofanyika  za  kumshamulia  mmoja  kati  ya  wote  waliotangaza  nia  ya  kuutaka  urais  wa  nchi  yetu.

Kwa  maana  hiyo  wanaofanya  mbinu  hizo  wanatuonyesha  ni  nani  wanayemuogopa  zaidi, pengine  kwa  uwezo  alionao  uliozidi  wengine, na  hivyo  kutufanya  tumtambue  anayefaa  kuichukua  nafasi  hiyo  kuu  katika  nchi  yetu.Naye  si mwingine, bali  ni Edward Ngoyai  Lowassa.

Hilo  linaletwa  na  ukweli  wa  asili  kwamba  kati  ya  miti  yote, mti  wenye  matunda  hupata  misukosuko  mingi  kama  kurushiwa  mawe  kila  wakati,kupandwapandwa  mara  kwa  mara, kutikiswatikiswa  mara  nyingi  na  kadhalika.

Lakini  jingine  ni  kwamba, kawaida  ni  vigumu  kuujua  ubaya  au  uzuri  wa  kitu  kabla  ya  kukilinganisha  kitu  hicho  na  vingine.

Mfano, wakati  Lowassa  alipolazimika  kujiuzulu  uwaziri mkuu, wapo  waliolichukulia  hilo  kwamba  ni  kuyakubali  yaliyotendeka  kuwa  ni  makosa  yake.

Lakini  baada  ya  kashfa  iliyokubwa  zaidi  ya  mara  mbili  ya  kashfa  iliyomuondoa  Lowassa  kutokea  na  karibu  kwa  mtindo  uleule, lakini  bila  kutokea  kitu  chochote  kwa  nafasi  kama  aliyokuwa  nayo Lowassa, ndipo  imejidhihirisha  kuwa  alichokifanya Lowassa  ni  kitendo  cha  uwajibikaji  wa  kijasiri.

Hicho  ni kitendo  kinachodhihirisha  ubora  wake  ambao  haukuonekana  kwa  wakati  huo  kwa  vile  haukuwa  na  mahali  pa  kuulinganisha  wala  kuufananisha.

Kitendo  cha  uwajibikaji  wa  aina  hiyo  kiliwahi  kuonyeshwa  na  mzee  Ali  Hassan  Mwinyi  wakati  huo  akiwa  waziri  wa  mambo  ya  ndani, ambaye  baadae  alikubaliwa  na  wananchi  kuwa  Rais.

Ikumbukwe  kwamba  kuwa  na  kiongozi  wa  nchi  asiyekubali  kuwajibika  ni  kitu  hatari  sana.

Hii  ni  kwa  sababu  anaweza  kufanya  lolote  kwa  kuwa  kimamlaka  hakuna  wa  kumfanya  lolote

Lakini  tukimpa  aliyewahi  kuonyesha  uwajibikaji  walau  tunakuwa  na  imani  ya  kuepukana  na  hatari  hiyo.Huo  ndio  ubora  mwingine  wa  Lowaasa

No comments:

Post a Comment