Majambazi hao pia wanadaiwa kuiba jenereta, redio, viti, betri ya gari na spika ya redio.
Akizunguzia tukio hilo jana, Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Morogoro, Leonard Paul alisema uporaji huo ulitokea usiku wa
Februari Mosi.
Kituo hicho ni cha tatu kuvamiwa mwaka huu baada
ya Kituo Kikuu cha Polisi Rufiji, Mkoa wa Pwani na Bukombe kuvamiwa na
majambazi na kuua polisi wawili na kupora bunduki saba na risasi 60.
Mwaka jana majambazi walivamia Kituo cha Polisi
Mkamba, wilayani Mkuranga, Pwani na kuua askari mmoja na mgambo wawili
kisha kupora bunduki tano na risasi 60.
Kadhalika, Juni mwaka jana, majambazi yalivamia
Kituo cha Polisi Bukombe na kuua askari wawili na kupora bunduki 10 na
risasi kadhaa.
Akizungumzia uvamizi huo, Kamanda Paulo alisema
baada ya wizi huo askari walianza msako na kufanikiwa kuipata bunduki
hiyo na risasi 30, viti vitatu, jenereta na redio vikiwa vimefichwa
katika pori la Simbangingile lililopo Mngeta Wilaya ya Kilombero.
Polisi inawashikilia watu watatu kutokana na tukio
hilo ambao ni Ramadhani Shewele (20), Hamisi Ahmed (45) na Ignus
Shewele (34) wote wakazi wa Nakagulu.
Alisema mtuhumiwa mmoja aliyetajwa kwa jina la Emmanuel Shewele (41) bado anatafutwa na polisi.
Kamanda Paul aliwaomba wananchi kutoa ushirikiano ili kuwapata watuhumiwa wengine.
Katika tukio jingine, dereva wa Mkuu wa Polisi
Wilaya ya Manyoni, Mkoa wa Singida, Aloyce Alibinus amefariki dunia
baada ya kujipiga risasi. Akizungumza kwa simu, Mkuu wa Polisi Manyoni,
Alute Makita alisema sababu za askari huyo kujiua hazijafahamika.
Alisema kuwa baada ya Alyoce kupewa bunduki hiyo, alikwenda nyumbani kwake na kufungulia radio kwa sauti kubwa.
No comments:
Post a Comment