Thursday, 4 June 2015

FIFA INAHITAJI MAGEUZI MAKUBWA ASEAMA BLATTER .... >>

                                                   
Aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Sepp Blatter amemaliza kwa aibu na fedheha miaka 17 ya utumishi wake uliotukuka.

Juzi, Blatter alitangaza kujiuzulu kwake. Katika hotuba yake fupi, Blatter alieleza:

“Nimekuwa nikitafakari kwa kina kuhusu urais wangu na miaka 40 ya maisha yangu nikiwa ndani ya shirikisho hili na mchezo wa soka.                
“Ninaipenda Fifa kuliko kitu chochote kingine, ninataka kila kitu kwa masilahi ya Fifa na soka. Nilifikiria kuomba kuchaguliwa tena kiongozi wa Fifa, niliamini kuwa hicho kingekuwa kitu muhimu kwa shirikisho. Uchaguzi ule umemalizika, lakini changamoto zinazoikabili Fifa bado zipo. Fifa inahitaji mabadiliko makubwa ya msingi.

                                               Йозеф Блаттер.jpg

“Nilikuwa nikitenda na kutimiza wajibu wangu kwa niaba ya wanachama wote wa Fifa, bila shaka ulimwengu wa soka mashabiki, wachezaji, klabu, watu wanaoishi, kupumua na kuipenda soka na kila tunachokifanya Fifa.

“Kwa hiyo, nimeamua kuweka chini mamlaka yangu kupitia mkutano mkuu maalumu. Nitaendelea kutimiza wajibu wangu kama rais hadi wakati ule wa uchaguzi.

“Nilitaka mkutano huo uwe Mei 2016 mjini Mexico City. Huo, ungekuwa wakati mzuri wa kutimiza yale tuliyokusudia, nilihisi kuwa ingekuwa ni kuendelea kuwapotezea muda mwingi, nikaiomba kamati ya utendaji iendeshe mkutano huo wa dharura wa mrithi wangu mapema iwezekanavyo. Hilo, lazima lifanyike kulingana na katiba ya Fifa na kutoa muda wa kutosha wa kupata wagombea wanaostahili ambao watajitokeza na kufanya kampeni.                
“Kwa kuwa sitakuwa mgombea, na kwa kuwa nitakuwa huru kutoka kwenye vikwazo ambavyo uchaguzi huo unatoa, nina hakika ya kuendeleza mabadiliko ya msingi, nikianzia na juhudi tulizozifanya. Kwa miaka mingi, tumejitahidi tuwezavyo kufanya mabadiliko ya kiuongozi, lakini inaonekana kwangu kwamba juhudi hizi lazima ziendelee, kwani hazitoshi.

“Kamati tendaji inao wawakilishi ya mashirikisho ya soka ambayo hatuna uwezo na mamlaka juu yake, lakini ambao kwa vitendo vyao, Fifa inahusishwa. Tunahitaji mabadiliko ya msingi.

“Ukubwa wa kamati tendaji lazima uangaliwe, upunguzwe na wanachama wake wachaguliwe kupitia mkutano mkuu wa Fifa. Lazima, tuangalie mienendo yao kwa kutumia chombo kimoja kinachosimamiwa na Fifa na siyo mashirikisho. Tunahitaji ukomo wa muda wao, siyo kwa rais pekee, bali wanachama wote wa kamati tendaji.

“Nimepigania mabadiliko yote, kila mmoja anajua, juhudi zangu zangu zimekwamishwa.

Safari hii, nitafanikiwa

No comments:

Post a Comment