Akizungumza jana, meneja wa timu hiyo, Enock Mwanguku alisema msimu ujao wa ligi timu hiyo itanolewa na Mayanga.
‘’Tayari, timu yetu imepata kocha mpya, Salum Mayanga baada ya kuondoka kwa Makata,” alieleza Mwanguku.
Msimu uliopita, Prisons ilianza kunolewa na David Mwamwaja aliyetimuliwa kazi baada ya timu hiyo kufanya vibaya na mikoba yake kuchukuliwa na Makata.
Mwanguku alisema wana imani kuwa ujio wa Mayanga katika timu hiyo utaiwezesha Prisons kuwa na matokeo mazuri kwani kocha huyo ni mzoefu katika soka nchini.
Wakati huohuo, timu hiyo inatarajia kuanza kambi Ijumaa kwa ajili ya kuanza usajili wa wachezaji wapya wakiwa tayari kwa msimu ujao wa Ligi Kuu.
Wakati huohuo, timu hiyo inatarajia kuanza kambi Ijumaa kwa ajili ya kuanza usajili wa wachezaji wapya wakiwa tayari kwa msimu ujao wa Ligi Kuu.
No comments:
Post a Comment