Ugiriki imetangaza kuchelewa kulipa
deni la Euro milioni mia tatu ambalo walitakiwa kulilipa shirika la
kimataifa la fedha la IMF siku ya Ijumaa.
Utaratibu huo ambao unaruhusiwa na kanuni za IMF,uliwahi kufanywa na nchi ya Zambia miongo mitatu iliyopita.
Mwandishi wa BBC wa masuala ya uchumi anasema mpango huo unaweza kuwa mbinu ambayo Ugiriki umeitumia ili kuweka msisitizo kwa wadeni wake wa kimataifa wakati huu nchi hiyo ikitafuta ufumbuzi wa madeni yanayolikumba taifa hilo.
No comments:
Post a Comment