Monday, 8 June 2015

YA LIVERPOOL ..<<>>

LIVERPOOL imekiri kukubaliana na mshambuliaji wa Burnley, Danny Ings, ili kutua katika timu hiyo kwa msimu ujao na sasa kinachosubiriwa ni vipimo vya afya. Ings, 22, alikuwa anawaniwa pia na Manchester United na Real Sociedad na mkataba wake ulikuwa unamalizika msimu huu na Liverpool wamefanikiwa kumtwaa. Taarifa iliyotolewa na Liverpool jana ilisema, timu hiyo imekubaliana rasmi na mchezaji huyo na kilichobaki ni vipimo vya afya kabla ya kutua rasmi. “Liverpool FC inapenda kutamka wazi imekubaliana mambo kadhaa na Danny Ings na mshambuliaji huyo atajiunga rasmi na klabu Julai 1, mara baada ya mkataba wake na Burnley kumalizika.

No comments:

Post a Comment