Friday, 13 February 2015

SHAMBULIO LA KWANZA LA BOKO HARAAM .. CHAD ! >>

 Magari ya jeshi la Chad yaliyotumwa Cameroon kupambana dhidi ya Boko Haram.
Shambulio hili limefanyika usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa wiki hii katika mji wa Ngouboua kando ya Ziwa Chad. Washambuliaji walisafiri eneo hilo wakitumia mitumbwi mitatu.

Watu kadhaa wameuawa akiwemo mkuu wa kijiji. Baada ya shambulio hilo, jeshi la Chad liliingilia kati na kuwatimua wanamgambo hao wa Boko Haram.
Kundi la Boko Haram, limeendesha shambulio hilo usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa wiki hii katika kijiji cha Ngouboua pembezoni mwa ziwa Chad, kilomita mbili na Nigeria, ambapo wanamgambo wa kundi hilo waliingia katika kijiji hicho wakitumia mitumbwi mitatu.

Wauaji hao walijigawa katika makundi mawili. Kundi la kwanza liliendesha shambulio dhidi ya ngome ya vikosi vya usalama, wakati ambapo kundi la pili lilikua likichoma mota shemu moja ya kijiji hicho cha Ngouboua, na kusababisha hofu miongoni mwa wakazi. Katika mapiagano hayo na vikosi vya usalama vya Chad, mwanajeshi mmoja ameuawa na wengine wanne wamejeruhiwa, kulingana na idadi iliyotolewa na jeshi la Chad. Upande wa raia wa kawaida, mkuu wa kijiji cha Ngouboua ameuawa na wakazi wengine watatu wamejeruhiwa.

Jeshi la Chad lililazimika kutumia ndege za kivita. Jeshi la Chad limebaini kwamba ndege zake za kivita zimeshambulia kwa mabomu mitambwi mitatu ambayo walikitumia katika usafiri kwa kuingia katika kijiji cha Ngouboua. Idadi ya wanajeshi na askari wa polisi imeongezwa katika kijiji hicho. Hata hivyo operesheni ya kuwasaka wanamgambo wa Boko Haram inaendelea.

No comments:

Post a Comment