Mkufunzi mpya wa timu ya Togo Tom
Saintfiet amemshtumu nahodha wa timu hiyo Emmanuel Adebayor kwa ukosefu
wa nidhamu baada ya mshambuliaji huyo wa Tottenham kushindwa kujiunga na
kikosi hicho kwa wakati ufaao kwa mechi ya ufunguzi ya kufuzu kwa kombe
la Afrika wikendi ijayo.
Mkufunzi huyo kutoka Ubelgiji alikuwa akizungumza kabla ya kuondoka kuelekea Togo ili kushiriki katika mechi ya kirafiki na Ghana siku ya jumatatu.
''Ni miongoni mwa wachezaji muhimu wa timu hii lakini siwezi kushirikiana nao iwapo hawako katika timu,ni lazima wawe na nidhamu kama wengine''.
Togo watacheza na Liberia mjini Lome siku ya jumapili katika mechi za kundi A .
Klabu ya Adebayor Tottenham ilimpatia likizo mara mbili msimu huu ili kurudi nyumbani na kusuluhisha maswala ya kibinafsi ambayo mshambuliaji huyo amelalamikia katika mitandao ya kijamii.
No comments:
Post a Comment