Rais wa Sudan Omar El Bashiri
amewabadilisha mawaziri wake wa Ulinzi,mafuta na maswala ya kigeni
katika mabadiliko makubwa tangu uchaguzi wa mwezi Aprili.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa kuondolewa kwa waziri wa Ulinzi Abdel Rahim Hussein ambaye ni mwandani wa rais huyo wa mda mrefu ni tukio ambalo halikutarajiwa.
Amepewa wadhfa wa chini kama Gavana wa jimbo la Khartoum.
Rais Bashir na Hussein wanasakwa na mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC kwa kutekeleza uhalifu katika eneo la Darfur.
No comments:
Post a Comment