Maafisa wa usalama wa Kenya wanasema wameweza kuunganisha uhuisano uliyopo kati ya bishara haramu ya pembe huko Asia na kufadhilwa kwa kundi la pwani linalotaka kujitenga la MRC.
Taarifa kutoka kwa waziri wa mambo ya ndani Joseph Nkaissery inaeleza kwamba, watu 14 wamekamatwa kuhusiana na shehena ya pembe za ndovu zilizosafirishwa hadi Thialand, na fedha kulipwa kundi linalopigania kujitenga kwa pwani la Mombasa Republican Council, MRC.
Wakuu wa kundi hilo lililopigwa marufuku, wanasisitiza kwamba lengo lao ni kutetea haki na uhuru wa waislamu wa Kenya. Imekanusha mara kwa mara kuhusika na mlolongo wa mahsmabulizi katika eneo la pwani la taifa hilo.
No comments:
Post a Comment