Uchina imetaja kama kukosa
kuwajibika ipasavyo kwa Marekani kudai kuwa wadukuzi wa Uchina ndio
waliosababisha udukuzi wa taarifa za ofisi za serikali ya Marekani.
Shirika la ujasusi la FBI chini Marekani linachunguza ni kwa namna gani wadukuzi wa komputa waliweza kuingilia taarifa hizo binafsi za wafanyakazi wa serikali wapatao milioni nne .
Ofisi ya utumishi ya nchini hiyo inasema karibu watu milioni nne ambao wanafanya kazi au waliwahi kufanya kazi wameathirika na udakuzi huo.
No comments:
Post a Comment