Saturday, 6 June 2015

Toka GP wameandika ....><><><><>< MAJUTO ATAPELIWA



Source GP
  CHANGA! Mkongwe kwenye sanaa ya vichekesho Bongo, Amri Athuman ‘Mzee Majuto’ amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kutapeliwa shilingi milioni mbili alizopaswa kulipwa kwenye shoo ya Instagram iliyofanyika hivi karibuni katika Viwanja vya Posta, jijini Dar.

 
Mkongwe kwenye sanaa ya vichekesho Bongo, Amri Athuman ‘Mzee Majuto’.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, wiki moja kabla ya shoo hiyo, mwigizaji Wema Sepetu  alimpigia simu Mzee Majuto aliyekuwa nyumbani kwake mkoani Tanga na kumpa ‘dili’ la kutokelezea kwenye shoo hiyo (special appearance) kwa maelewano ya malipo ya shilingi milioni mbili taslimu.

“Mzee Majuto alionekana kwenye shoo hiyo akiwa kama staa mualikwa akiwa na mchekeshaji mwenzake Stan Bakora pamoja na Wema mwenyewe ambapo mbali na uwepo wao katika pati hiyo walitakiwa kufanya kazi kama vile kuchekesha mashabiki wao.

“Baada ya shoo kuisha na kila mtu kula zake, Mzee Majuto alimuulizia Wema kuhusu mkwanja wake lakini hakupata majibu yaliyoeleweka wakati wenzake wote wakiwa wameshalipwa chao.

“Wema alishangazwa na ishu hiyo ndipo alipomtafuta muandaaji wa shoo (Fredy  Mgimba ‘Frekon’) lakini aliingia mitini jambo lililomfanya Wema avujishe siri kwenye ukurasa wake wa Instagram akidai kuwa waandaaji wa Instagram Party wamemfanya aonekane vibaya kwa kutomlipa Mzee Majuto fedha zake na kuongeza kuwa hatofanya nao kazi tena,” kilisema chanzo chetu.

Baada ya kunyaka ubuyu huo kutoka kwa chanzo chetu, waandishi wetu walianza ‘kumvutia waya’ Mzee Majuto ambaye alikiri kupewa dili hilo kupitia kwa Wema na kudai waandaaji ‘wamemuingiza mjini’.

“Hao wamenidhulumu kwa kuwa mimi ni mzee na wamenitumikisha usiku mzima bila kunipa chochote, sawa tu hakuna shida. Sitakwenda kushitaki popote, namwachia Mungu,” alisema Majuto.
Alipotafutwa muandaaji (Fredy), simu yake iliita muda mrefu bila kupokelewa na baadaye alipokea na kuomba apigiwe baada ya muda kidogo kwa kuwa anaendesha gari.

Baada ya nusu saa, mwandishi wetu alimpigia simu kwa nyakati tofauti lakini hakupokea tena.

No comments:

Post a Comment