Waziri wa michezo wa Afrika Kusini ,
Fikile Mbalula, sasa anasema rais wa zamani wa Afrika kusini Thabo
Mbeki ndie aliyeruhusu ulipwaji wa fedha ,dola milioni 10 kwa FIFA ,
hela ambayo sasa inakumbwa na madai kwamba ilikuwa rushwa .
Lakini waendesha mashtaka wa Marekani wanadai ilikuwa hongo, iliyoshawishi kupewa uenyeji wa kombe la dunia mwaka 2010 .
Bwana Mbeki mwenyewe hajatoa kauli yoyote kuhusiana na swala hilo.
Barua inayosemekana iliandikwa na shirikisho la soka nchini Afrika kusini , inaonekana kuongeza uzito kwenye shutuma kwamba serikali ya nchi hiyo ilitoa malipo hayo kwa siri.
No comments:
Post a Comment