Ofisi ya Utumishi wa nchini humo imesema, takriban watu milioni nne
ambao wanafanya kazi au waliwahi kufanya kazi wameathirika na udukuzi
huo.
Idara ya Utumishi ya Serikali ya Marekani inayosimamisha huduma za
wafanyakazi wa umma nchini humo imefanya uchunguzi wa usalama wa taarifa
za wafanyakazi wake wapatao milioni nne.
Idara hiyo inasema wadukuzi hao walingilia taarifa hizo kwa njia ya
mtandao tangu mwezi Aprili jambo linalofanyiwa uchunguzi na Shirika la
Kijasusi la FBI.
Taarifa zote za udukuzi huo na idadi ya watu waliohusika bado
haijafahamika lakini ofisa mmoja anasema kila idara ya serikali itakuwa
imeathirika kwa kiasi kikubwa.
Mjumbe wa Kamati ya kiintelejensia ya baraza la Seneti imewalaumu wadukuzi kutoka nchini China kwa kuhusika na udukuzi huo.
Hii sio mara ya kwanza kwa taarifa muhimu kama kama hizo kufanyiwa udukuzi.
Mwezi Machi mwaka jana, wadukuzi walijaribu kuwadukua wafanyakazi wa
serikalini ambapo pia mwezi Novemba taarifa za wafanyakazi wa Wizara ya
Mambo ya Ndani wapatao 20,000 zilidakuliwa.
Taarifa zaidi kutoka wizara ya usalama nchini Mrekani zinasema kuwa,
uhalifu huo umezidi sana hasa kuanzia mwanzoni mwa mwezi huu.
No comments:
Post a Comment