Stori:
Katika hali isiyo ya kawaida Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zachary Kakobe amefunguka na Injili nzito kwa kuwataja baadhi ya wagombea urais kwamba waingie katika wokovu kamili badala ya kuwa na wokovu aliodai ni wa kuigiza.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zachary Kakobe.
“Leo sikwepeshi maneno. Kila mtu anajifanya ameokoka lakini huo ni wokovu ule. Nyalandu (Lazaro), ameokoka kweli? Mwigulu (Nchemba), ameokoka kweli, Mwakyembe (Dk. Harisson) ameokoka? Angalia sasa kwa viwango hivi ndiyo utajua umeokoka au namna gani.
Lazaro Nyalandu.
Nyalandu aliwahi kuonekana katika kanisa linaloongozwa na Nabii Josephat Mwingira Kibaha ambako aliwaomba waumini kumuunga mkono katika harakati zake za urais na Dk. Mwakyembe aliwahi kuonekana katika Kanisa la Askofu Josephat Ngwajima.
Hata hivyo, Mwigulu naye kwa mujibu wa Askofu Kakobe, amekuwa akijitangaza kwamba ameokoka, wokovu ambao kiongozi huyo haridhiki nao.Hakuna kiongozi yeyote kati yao aliyepatikana juzi kuzungumzia wito huo wa Askofu Kakobe.
No comments:
Post a Comment