OHOOO! Wakati Nasibu Abdul ‘Diamond’ akijinadi kwa mbwembwe kuwa anategemea kiumbe kutoka kwa mwandani wake Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’, ubuyu mpya wa mjini unadai kuwa mimba aliyobeba mrembo huyo si ya Diamond, Amani limemeza sababu za kutosha.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilicho karibu na Diamond anayesumbua kwa sasa na wimbo wake wa Nana, tangu habari ya ujauzito wa mlimbwende huyo mwenye asili ya Uganda ianze kupamba vyombo mbalimbali vya habari, watu walio karibu na staa huyo hawakuziamini.
“Hatukuamini sababu kwanza muda ambao Diamond alikutana na Zari ulikuwa mchache ukilinganisha na miezi mitatu ambayo mimba ilibainika. Watu wa karibu tulikuwa tunajua lakini tulikuwa tunashindwa pa kuanzia kusema.
MITANDAO YAWASAIDIA
“Sijui bwana nani alivujisha hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii ndiyo maana hata sisi sasa tukawa radhi kufunguka. Tena imeeleza mambo ya ukweli tupu ambayo sisi tulikuwa tunayajua,” kilisema chanzo chetu.
IMESEMAJE MITANDAO?
Watumiaji mbalimbali wa mitandao ya kijamii wametoa maoni kuwa, kwa asilimia 90 mimba ya Zari si ya Diamond na kuna uwezekano ana tatizo la uzazi kwani hata mpenzi wake wa zamani, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ aliwahi kukaririwa akisema Diamond hajampa ujauzito kama yeye alivyokuwa akijisifia kuwa amempa halafu ukatoka.
ANA TATIZO?
“Yawezekana ana matatizo. Haiwezekani aseme amempa mimba Jokate akaitoa halafu mwenyewe akatae. Kama mnakumbuka hata alipomwagana na Penny (Penniel Mungilwa), alisema ametoa mimba yake kitu ambacho mrembo huyo alikikanusha na kumtaka kama kweli ana ushahidi wa hospitali aliyoitumia kutoa mimba ampe,” alieleza mdau mtandaoni.
MWINGINE AKUMBUSHIA YA MUME WA ZARI
Kama hiyo haitoshi, mchangiaji mwingine katika mitandao hiyo ya kijamii alishibisha hoja ya mimba ya Zari si ya Diamond kwa kukumbushia suala la aliyekuwa mume wa Zari, Ivan Semwaga kufunguka kuwa kamwe Zari hawezi kumzalia Diamond.
“Mume wa Zari alikuwa anaujua ukweli wa mimba ya Zari (huenda ni yake) ndiyo maana alinukuliwa katika vyombo mbalimbali vya habari pasipokuwa na shaka yoyote, kama hamuamini, akijifungua kipimo cha DNA kitamaliza ubishi,” alichangia mtu huyo.
Zari akiwa na Katunzi.
KATUNZI ATAJWA
Ushahidi wa mimba hiyo kuwa si ya Diamond ulizidi kumwagwa mtandaoni kuwa Diamond hakuwa mtu wa kwanza kuonana Zari kwani alitanguliwa na mfanyabishara maarufu Bongo, Mzamili Katunzi ambaye inasemekana ndiye aliyemfata Bongo kisha baadaye akakutana na Diamond.
“Mtu akiniambia hiyo mimba ni ya Katunzi naweza nikakubali sababu ndiyo mtu wa kwanza kukutana na Zari lakini Diamond hana chake pale, si unakumbuka Global (Kampuni ya Global Publishers) waliwahi kutoa picha ya zamani ya Katunzi akiwa na Zari? Tujiongeze,” alichangia mchangiaji mwingine mtandaoni.
KATUNZI ANASEMAJE?
Mwanahabari wetu alimtafuta Katunzi kujua anazungumziaje kutajwa kwenye ujauzito huo ambapo alijibu kwa kifupi:
“Nani kawaambia? Hivi si mnajua mimi nina familia yangu? Kwa nini msimuulize mama kijacho mwenyewe (Zari). Mama mtoto ndiye anayejua ukweli wote.”
DIAMOND SASA
Kwa upande wake Diamond alipotafutwa na mwanahabari wetu juu ya habari hiyo, alisema maneno kwamba mimba si yake si mageni lakini hayatilii maanani sababu hayana ukweli wowote.“Watu tu wenye roho mbaya ndiyo wanaongea maneno hayo, ninavyojua mimi tumbo lile linanihusu kwa asilimia mia moja,” alisema Diamond.
No comments:
Post a Comment