Monday, 8 June 2015

RUSSIA YAONYWA NA G7 ....

  Rais wa Russia Vladimir Putin

Kundi la nchi saba zenye utajiri wa kiviwanda duniani zimeonya Russia kwamba zitaongeza vikwazo zaidi vya kiuchumi dhidi yake.

Zimesema kama Moscow isipotekeleza makubaliano ya sitisho la mapigano ili kumaliza mgogoro mashariki mwa Ukraine baina ya waasi wanaounga mkono Russia na vikosi vya Kyiv.

Rais wa marekani Barack Obama amesema kuna makubaliano yenye nguvu kutoa shinikizo kwa Russia kutokana na kujihusisha kwake katika mgogoro wa Ukraine na kupokonya kwa nguvu mwaka jana peninsula ya Ukraine, Crimea.

Bwana Obama amesema swali kwa rais wa Russia, Vladmir Putin ni kama anataka kuendelea kuharibu uchumi wa nchi yake kutokana na maamuzi mabaya ya kutengeneza sifa za  utaifa kwa kuendelea kusaidia waasi au kuheshimu utaifa wa Ukraine.

No comments:

Post a Comment