Uongozi wa klabu ya Simba umeagizwa
kuanza mazungumzo mapya na mchezaji Ramadhani Singano (Messi) baada ya
mvutano wa utata wa mkataba wake.
Kwa mujibu wa Afisa mawasiliano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto, TFF imekutana na uongozi wa klabu ya Simba SC ukiwakilishwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Collin Frisch na mchezaji Ramadhani Yahya Singano aliandamana na uongozi wa Chama cha Wacheaji wa Mpira wa Miguu (SPUTANZA) katika kutafuta suluhu ya jambo hilo.
Kizuguto alisema kikao hicho kiliitishwa na TFF ili kujadili na kutafuta ufumbuzi wa utata wa kimtakabta kati ya mchezaji na klabu ya Simba.
Amesema katika kikao cha leo (Jumanne) pande zote zimeeleza kutambua utata ulio ndani ya mikataba iliyokuwepo ambayo kimsingi iliingiwa kabla ya uongozi wa sasa wa Simba SC.Amesema kuwa kwa pamoja, pande hizo mbili zimekubaliana kuanza mazungumzo ya makubaliano mapya na hatimaye mkataba mpya utakaoanza katika msimu mpya wa 2015/16.
No comments:
Post a Comment